SIMBA YAJA NA GAZETI LAKE

Klabu ya Simba imeanzisha gazeti lake litakaloitwa ‘Simba Nguvu Moja’ ambalo litatumbulishwa rasmi siku ya Jumatano.

Gazeti hilo litakuwa linaandikwa habari za Michezo na Burundi ambapo litakuwa linatoka mara moja kwa wiki siku ya Jumamosi.

Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Hajji Manara amesema kumekuwa na magazeti mengi yaliyokuwa yanatumia jina na nembo ya Simba huku klabu hainufaiki chochote.

Manara amesema gazeti hilo litapatikana nchi nzima na bei yake itakuwa shilingi 500.

“Klabu ya Simba imeanzisha gazeti litakaloitwa Simba Nguvu Moja litakuwa linatoka kila siku ya Jumamosi kwa shilingi 500,” alisema Manara.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *