Simba Yakamata Kiraka wa Mtibwa, Nyota Kadhaa Kufuata

KLABU ya Simba imeendelea na zoezi la usajili kwa kasi ya ajabu baada ya leo tena kumsainisha nyota mwingine kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao.

Kiraka wa Mtibwa Ally Shomari mwenye uwezo wa kucheza nafasi kadhaa uwanjani zikiwemo za ulinzi zote na winga amesaini mkataba wa miaka miwili hivyo kujumuika na nyota wengine kadhaa wapya waliosajiliwa kulinda heshima ya Simba kwenye michuano ya kitaifa na kimataifa.

Ally Shomari akisaini mkataba mbele yamakamu wa Rais wa Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’

Simba ilijaribu kumsajili Shomari wakati wa dirisha dogo lakini mpango huo uliishia njiani lakini kwa kuonyesha walikuwa ‘serious’ na uhamisho huo, wekundu hao wamemaliza mchakato mapema baada ya dirisha kubwa kufunguliwa usiku wa kuamkia leo.

Kwasasa Simba inatajwa kumfukuzia kiungo wa kutumainiwa wa Yanga, Haruna Niyonzima na straika wa Nkana Red Devils, Walter Bwalya huku ‘deal’ ya Emmanuel Okwi ikionekana kama vile ilimalizika muda mrefu.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *