Simba yaleta msaidizi mpya wa Omog.

Uongozi wa klabu ya Simba umemtambulisha Masud Djuma raia wa Burundi na aliekua kocha mkuu wa klabu ya Rayon Sports nchini Rwanda kama kocha msaidizi atakaeshirikiana na mwalimu mkuu Marius Omog. Simba imefikia hatua hiyo baada ya aliekua kocha msaidizi Jackson Mayanja kuachia ngazi katika nyadhifa hiyo kutokana na sababu za kifamilia.

Masud Djuma anakuja kuinoa klabu ya simba baada ya kuipatia ubingwa klabu ya Rayon katika ligi kuu nchini Rwanda na kuchaguliwa kuwa kocha bora katika msimu wa mwaka 2016/17. Djuma ameahidi kazi zaidi kwenye nafasi iliyoacha wazi na Mtangulizi wake Jackson Mayanja.

“Mimi sina maneno mengi ya kuongea nimekuja kufanya kazi na siwezi kuahidi maajabu kwakua nimekuja kufanya kazi”
alisema Djuma

Simba inayojiwinda na mchezo wake dhidi ya Njombe Mji utakaochezwa katika dimba la Uhuru kabla ya kuvaana na watani wao wa jadi Yanga hapo Oktoba 28, imefikisha alama 12 baada ya kushinda michezo 3 na kutoa sare michezo 3 ikiwa mbele ya mahasimu wao Yanga kwa tofauti ya mabao.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *