SIMBA YALIA NA WAAMUZI VPL

Uongozi wa klabu ya Simba umeandika barua kwa bodi ya ligi, Serikali na chama cha waamuzi Tanzania kulalamikia kuhusu kunyimwa haki katika michezo yao ya ligi ya Vodacom.

Malalamiko hayo yanakuja siku tatu baada ya Wekundu hao kulazimishwa sare ya bao moja na watani wao Yanga katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.

Msemaji wa klabu hiyo Hajji Manara amewaambia waandishi wa habari kuwa wamechukua maamuzi hayo ili kutafuta haki kutokana vitendo vya waamuzi kupendelea wapinzani wao mara kwa mara.

Manara ameonyesha picha za video katika mechi dhidi ya Yanga wakinyimwa penati mbili, na matukio mengine katika michezo dhidi ya Mbao pamoja na ule wa Stand United.

Tumeandika barua kwa bodi ya ligi kulalamikia maamuzi katika mechi dhidi yetu, wamekuwa wakitoa maamuzi ya kutukandamiza mara kwa mara,” alisema Manara.

Simba itaelelekea mkoani Mbeya kujiandaa na mchezo dhidi ya Mbeya City utakaopigwa katika dimba la kumbukumbu ya Sokoine tarehe 5 Novemba.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *