Simba yamtangaza katibu mkuu mpya

KLABU ya Simba imemteua msomi Dk Arnold Kashembe kuwa katibu mkuu wake baada ya kamati ya utendaji kukutana jana jijini Dar es Salaam na uteuzi huo umeanza mara moja.

Dk. Kashembe ambaye ana shahada ya uzamivu aliwahi kuwa mhadhiri katika vyuo vikuu mbalimbali ndani na nje ya nchi anachukua nafasi iliyoachwa wazi kwa muda mrefu na Patrick Kahemele aliyehamia kampuni ya Azam Media.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari ya klabu hiyo, Kamati hiyo ilikutana jana na kuamua kujaza nafasi hiyo muhimu kwa uendeshaji wa masuala mbalimbali ya klabu.

Dr. Arnold Kashembe

Kamati hiyo imepanga kufanya mkutano mkuu wa kawaida Agosti 13 na wiki moja baadae watafanya Mkutano mkuu utakaojadili mabadiliko ya katiba.

Mikutano hiyo imeitishwa kwa kuzingatia takwa la kikatiba ya klabu linalotaka notisi ya kuitishwa mikutano hiyo,ifanywe sio chini ya siku 30 kabla ya mikutano yenyewe.

Wakati huo huo uongozi wa klabu umewaomba wanachama na mashabiki wake kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho shauri la viongozi wao wakuu linaendelea Mahakamani.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *