SIMBA YAOMBA SAPOTI YA MASHABIKI FAINALI SPORTPESA

Mabingwa wa Tanzania timu ya Simba imewaomba mashabiki wao kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa fainali ya SportPesa Super Cup dhidi ya Gor Mahia utakaopigwa kesho saa 9 alasiri.

Wekundu hao wamejipanga kuhakikisha wanarejea nyumbani na taji hilo lakini wameomba sapoti kwa mashabiki wao ili kutimiza lengo hilo.

Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Hajji Manara amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kuongeza hamasa uwanjani kwakua wapinzani wao wapo nyumbani hivyo watakuwa na hazina kubwa ya mashabiki.

Manara amesema wachezaji wapo katika hali nzuri na morali ipo juu wakiwa tayari kwa mpambano huo na wameahidi kutwaa taji hilo.

“Kikubwa ni mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu, mchezo utakuwa mgumu lakini wamejipanga kushinda na kurejea na kombe Tanzania,” alisema Manara.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *