Simba yatonesha ‘donda’ la miaka mitatu

TIMU ya Simba imekumbusha maumivu ya miaka mitatu iliyopita kwa Maafande wa Ruvu Shooting kufuatia kipigo kikubwa cha mabao 7-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom huku mshambuliaji Emmanuel Okwi akifunga mabao manne peke yake kwenye uwanja wa Uhuru.

Ruvu iliwahi kupokea kipigo kama hicho toka kwa mabingwa watetezi wa ligi kuu timu ya Yanga Februari 22, 2014 hivyo Simba imekumbusha machungu ya maafande ya miaka mitatu iliyopita.

 

Okwi akipongezwa na Erasto Nyoni baada ya kufunga moja ya mabao yake

Kabla ya mchezo huo msemaji wa Maafande hao Masau Bwire alijinasibu kuwafunga Wekundu hao huku akisema timu hiyo imebaki jina sio ile ya zamani lakini kipigo hicho kimemfanya kiongozi huyo kukosa la kusema.

Katika mchezo huo Simba ilitawala karibia mchezo mzima huku ikipata mabao matano kipindi cha kwanza ambapo Okwi alipiga ‘hattrick’ ndani ya dakika 17 wakati Shiza Kichuya na Juma Liuzio wakifunga mengine mawili dakika za 42 na 45.

Shiza Kichuya kushoto akimtoka mlinzi wa Ruvu Shooting

Mabao mengine ya Simba yalifungwa kipindi cha pili kupitia kwa Okwi tena na beki Erasto Nyoni ambaye alihusika pia katika upatikanaji wa mengine mawili katika mchezo huo.

Kiungo Haruna Niyonzima alishindwa kuendelea na mchezo huo baada ya kufanyiwa madhambi na mchezaji wa Ruvu na kutolewa kwa machela dakika ya 42.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *