SIMBA YAUNGURUMA TANGA.

NA MWANDISHI WETU, Tanga

????????????????????????????????????

KIKOSI cha timu ya soka Simba kimeanza vizuri ligi kuu ya msimu huu baada ya jioni ya leo kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya African Sports ya jijini hapa.

Bao hilo pekee la mchezo liliwekwa kimiani na mshambuliaji wake Kiganda, Hamis Kiiza ‘Diego’, aliyepokea pasi nzuri na nahodha Mussa Hassan ‘Mgosi’ dakika ya 57 ya mchezo.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, jijini hapa ulikuwa na kasi muda mwingi na kufanya mwamuzi Jacob Andogo wa Mara kutoa kadi nyingi za njano na kuwaonya wachezaji mara kwa mara.

Mchezo huo uliokuwa wa kukaminiana kwa wachezaji ulikusanya mashabiki wengi uwanjani hapa.

Wakati mchezo huo ukiwa unaenda timu hizo zilifanya mabadiriko kadhaa ya wachezaji kwa ajili ya kuimarisha vikosi vyao.

Washambuliaji wa African Sports Hussen Amir na Mendy James, itabidi wajilaumu wenyewe baada ya kukosa nafasi za kufunga kwenye dakika za mwishoni mwa mchezo.

Simba: Manyika Peter, Hassan Kessy, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Mursheed, Justice Majabvi, Awadh Juma, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto / Simon Sserunkuma, Mgosi, Kiiza / Boniface Maganga na Peter Mwalyanzi.

African Sports: Yussuph Yussuph, Raheem Juma, Novart Lufunga, Ayoub Mrisho, Hassan Matenela, Juma Shemvuni, Michael Mwaita, Pera Mavoi / Bakari Masoud, Mendy / Ally Ramadhan.

Michezo mingine iliyochezwa leo ilimalizika kwa Majimaji ya Songea kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu, huku Azam FC wakiwatambia Tanzania Prisons kwa kuwafunga mabao 2-1.

Mbneya City, wameshindwa kufurukuta nyumbani na kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar, huku timu za Ndanda FC na Mgambo JKT ziokitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1. Mtibwa Sugar imeweza kuitambia Stand United na kuifunga bao 1-0.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *