SINGIDA YAIKAMUA KAKAMEGA, YACHUKUA NAFASI YA TATU SPORTPESA

Singida United imeibuka mshindi wa tatu katika michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Kakamega Homeboyz kwa mikwaju ya penati 4-1.

Singida ilitoka nyuma bao moja na kusawazisha bao hilo kufuatia jitihada kubwa walizofanya vijana hao wa kocha Hemed Moroco.

Kakamega walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya nne kupitia kwa Wycliff Opondo baada ya walinzi wa Singida kuchelewa kuondoa hatari.

Baada ya bao hilo Singida walizinduka na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Kakamega lakini walienda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao hilo.

Danny Lyanga aliisawazishia Singida bao hilo kwa kichwa dakika ya 63 baada ya kupokea krosi safi upande wa kulia kutoka kwa Miraji Adam.

Penati za Singida zilifungwa na Deus Kaseke, Miraji, Shafik Batambuze na Lyanga.

Muda mfupi kutoka sasa mchezo wa fainali ya michuano hiyo kati ya Gor Mahia dhidi ya Simba utaanza.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *