SOMA USHAURI ALIOPEWA GIROUD NA KOCHA WA UFARANSA

Mshambuliaji Olivier Giroud ameambiwa anatakiwa kupata mechi nyingi katika timu yake ya Arsenal ili kuwepo kwenye kikosi cha Ufaransa kitakacho shiriki michuano ya kombe la dunia mwakani.

Giroud amekuwa chaguo la pili mbele ya Alexandre Lacazette akiwa hajaanza mechi yoyote ya ligi kuu mpaka sasa.

Giroud 31, alijiunga na Arsenal akitokea Montpellier mwaka 2012 alihusishwa na kutaka kujiunga na Everton, West Ham na Marseille majira ya joto yaliyopita kabla ya kuamua kubaki kwa Washika bunduki hao wa London.

Kocha mkuu wa Ufaransa Didier Deschamps anamuona Giroud ambaye amefunga mabao 29 katika michezo 69 ya timu ya taifa ila anahitaji kupata mechi nyingi ili amjumuishe kwenye kikosi kitakachoenda nchini Urusi.

Kocha msaidizi wa Ufaransa Guy Stephan amesema “Didier ana nafasi ya kuongea sasa na Olivier ili atafute suluhisho katika wiki chache zijazo. Hata kama itakuwa ni kutolewa kwa mkopo hilo ni juu yake.

“Olivier ni mchezaji mzuri kwetu, katika miezi ya karibuni amekuwa na uwiano mzuri wa kufunga ila anapaswa kucheza mechi nyingi,” alisema Stephen.

Giroud amefunga mabao matano katika mechi 21 za Arsenal msimu huu ukiwemo katika mchezo walioshinda mabao 5-0 dhidi ya Huddersfield.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *