Stars tayari kuingia Kambini kuwawinda Malawi

KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kesho anatarajia kuanza mazoezi rasmi na kikosi chake alichokitaja hivi karibuni,kujianda na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Malawi utakaochezwa jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma hili,

“Baadhi ya wachezaji wameanza kuripoti kwa ajili ya kambi hiyo na wameshaanza vipimo kwa ajili ya Afya zao” alisema Afisa habari wa shirikisho la soka nchini (TFF )Alfred Lucas, aidha Lucas amesema wachezaji wote walioko Simba pamoja wale wakimataifa wanatarajiwa kuwasili kesho na kukamilisha vipimo kabla ya kuanza kambi hiyo.

Nahodha Mbwana Samatta ni moja kati ya wachezaji wanaotarajiwa kuwasili kesho majira ya alfajiri akitokea nchini Belgium.

Alfred Lucas amesemea Maandalizi yote yamekamilika na ni imani ya TFF pamoja benchi la Ufundi kwa mambo hiyo itasaidia kuibuka na ushindi Kwenye mchezo huo.
Kikosi kamili cha Stars kitakachoimgia kambini [Caption]

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *