TAMBWE, KAMUSOKO KUREJEA DIMBANI KESHO

Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu nyota wa kimataifa wa mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga Amiss Tambwe na Thaban Kamusoko wataanza mazoezi kesho baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakiwakabili.

Tambwe raia wa Burundi bado hajacheza mchezo wowote wa ligi msimu huu mpaka sasa kutokana na majareha hayo huku Kamusoko akicheza mechi chache za mwanzo.

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga, Dismas Ten amesema amepokea taarifa kutoka kwa daktari wa klabu hiyo kuwa nyota hao wataanza mazoezi kesho pamoja na wenzao kujiandaa na michezo ijayo ya ligi.

“Wachezaji wetu Tambwe na Kamusoko wataanza mazoezi kesho baada ya kupona majeraha yao yaliyo waweka nje ya uwanja kwa muda mrefu, ni matumaini yetu wataanza kuonekana katika mechi zetu zijazo,” alisema Ten.

Baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa mabingwa hao watawakaribisha Mbeya City kwenye mchezo utakayofanyika kwenye uwanja Uhuru, Novemba 19.

Nyota hao wanatarajiwa kuwepo kwenye mchezo huo kama kocha George Lwandamina ataona inafaa.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *