TARIMBA AAMUA KUJIWEKA PEMBENI YANGA

Mwenyekiti wa kamati ya mpito wa klabu ya Yanga, Abbas Tarimba ameamua kujiweka pembeni katika nafasi yake kutokana na sintofahamu miongoni mwa viongozi wa timu hiyo.

Maamuzi hayo yamekuja siku moja baada ya mkutano wa wenyeviti wa matawi kukutana na Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga na kuiponda kamati hiyo ilichaguliwa katika mkutano mkuu uliopita.

Tarimba alitoa maamuzi hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha michezo cha Radio Uhuru huku akiweka wazi itakuwa ngumu kwa mabingwa hao kupiga hatua kama wataendelea kuwa na viongozi hao.

Kiongozi huyo wazamani wa Yanga ameongeza kuwa hakuna umoja ndani ya klabu hiyo ndio maana hakushirikishwa katika kikao cha jana cha Wenyeviti wa matawi ambacho waliijadili kamati yao wakisema haijafanya kazi yoyote hali iliyopelekea kujiweka pembeni.

“Binafsi nimeamua kujiweka pembeni katika kamati ya mpito ya Yanga kutokana na mambo yanayoendelea ndani ya klabu kwa ajili ya maslahi na furaha ya Wanayanga,” alisema Tarimba.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *