TFF YAMPA ONYO CANNAVARO

NA MWANDISHI WETU
cannavaro
BAADA ya nahodha wa timu taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ na klabu ya Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuonekana katika gazeti moja la michezo nchini akiwa na jezi za Yanga, huku akishika picha Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limetokeza na kusema limebaini kuwepo kwa vitendo vyaa wanafamilia wa mpira wa miguu kujihusisha na masuala ya siasa wakiwa katika mavazi rasmi ya mpira ambayo yana nembo za vilabu na wadhamini wa Ligi.
Katiba ya TFF ibara ya I (4) inatamka “TFF is neutral in matters of politics and religion.
Discrimination of any kind against a country, private person or group of people on account race, skin colour, ethnic, national or social origin, gender, language, religion, political opinion or any other opinion, wealth, birth or any other status is strictly prohibited and punishable by suspension or expulsion.”
Aidha kanuni za Ligi, Kanuni ya 14(40) inatamka: “ Hairuhusiwi kwa mchezaji, mwamuzi au kiongozi wa timu kuonyesha kwa njia yeyote tangazo au ujumbe unaohusiana na dini yeyote au ulio na madhumuni maalum bila idhini ya TFF/TPLB”.
Taarifa iliyotumwa leo mchana na Ofisa Habari wa shirikisho hilo ilisema kuwaa TFF, inachukua fursa kuwakumbusha wana familia wote wa mpira wakiwemo viongozi, wachezaji, waamuzi, makocha na madaktari wa michezo kuwa ni marufuku kuelezea hisia zao za kisiasa au kujihusisha katika kampeni za kisiasa wakiwa katika mavazi rasmi ya mpira zikiwemo jezi na track suites zenye nembo za TFF, vilabu wadhamini na ligi, Taifa stars au za washirika wa TFF wakiwemo wadhamini.
Aidha ni marufuku kwa mashabiki wa mpira kutumia fursa ya mechi za mpira wa miguu kubeba mabango au kusambaza ujumbe wa kisiasa.
Hatua kali zitachukuliwa kwa wataokiuka mahitaji ya katiba na kanuni za mashindano. TFF inatambua haki za wanamichezo kushiriki katika siasa ili mradi ushiriki wao hazikiuki kanuni na mahitaji ya katiba za TFF na FIFA.
It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *