TIMU 8 ZATANGULIA 16 BORA ULAYA

Timu nane zimefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kumaliza nafasi mbili za juu kwenye makundi yao.

Timu hizo zimetoka katika kundi A hadi D ambapo nyingine nane zitakazoungana nazo zitapatikana kesho baada ya kumalizika mechi nyingine nane.

Timu zilizofuzu ni Manchester United, FC Basel, PSG, Bayern Munich, AS Roma, Chelsea, Barcelona na Juventus.

Droo ya hatua ya 16 bora inatarajiwa kufanyika jijini Nyon, Uswis siku ya Jumatatu.

Matokeo ya mechi zote za UCL

Benfica 0-2 Basel

Man United 2-1 CSKA Moscow

Bayern Munich 3-1 PSG

Celtic 0-1 Anderlecht

Chelsea 1-1 Atletico Madrid

Roma 1-0 Qarabag FK

Barcelona 2-0 Sporting CP

Olympiacos 0-2 Juventus

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *