TSHABALALA: TUPO TAYARI KWA FAINALI

Nahodha msaidizi wa timu ya Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ amesema wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa fainali wa SportPesa Super Cup kesho dhidi ya Gor Mahia.

Simba haipewi nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo kutokana na ubora walionao Gor ambao ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

Tshabalala amesema wachezaji wana morali ya hali ya juu na kila atakayepata nafasi ya kucheza yupo tayari kupeperusha vyema bendera ya Simba.

Mlinzi huyo ameongeza kuwa wanafahamu umuhimu wa kuchukua ubingwa huo kuwa itakuwa ni heshima kwa nchi na kwao pia kwakua watapata tiketi ya kwenda Uingereza kucheza na Everton.

“Tunauchukulia mchezo kwa umuhimu mkubwa, wachezaji wote tuna morali ya hali ya juu tunamuomba Mungu atuamshe salama tukiwa na afya nzuri ili tufanye vizuri,” alisema Tshabalala.

Katika mchezo huo kiungo Haruna Niyonzima ataukosa kutokana na kuwa na kadi mbili za njano.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *