TSHISHIMBI, AJIB KUIKOSA RAYON KESHO

Kaimu kocha mkuu wa timu ya Yanga, Noel Mwandila amethibitisha kuwa nyota Papy Tshishimbi na Ibrahim Ajibu hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi Rayon Sports.

Tshishimbi alipata majeraha katika mchezo wa Wolaita Dicha ingawa alicheza mchezo wa watani wa jadi Simba, Aprili 29 na kutolewa kipindi cha pili.

Mwandila amesema kuhusu Ajibu anajua ana matatizo ya kifamilia huku akisisitiza Meneja Hafidh Saleh ndio ana nafasi ya kuliongelea zaidi suala hilo.

Kocha huyo amesema maandalizi yanaendelea vizuri na wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo ambao wanatakiwa kushinda ili kufufua matumaini ya kuingia nusu fainali.

“Kesho tutawakosa Tshishimbi na Ajibu lakini wengine wote wapo katika hali nzuri, tunategemea mchezo mgumu lakini tumejipanga kushinda,” alisema Mwandila.

Wachezaji Obrey Chirwa, Thaban Kamusoko na Amiss Tambwe wanatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka dimbani kesho baada ya kupona majeraha.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *