TSHISHIMBI MCHEZAJI BORA VPL MWEZI FEBRUARI

Kiungo wa mkabaji wa timu ya Yanga Papy Tshishimbi ameibuka kidedea baada ya kuchaguliwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mwezi wa Februari.

Raia huyo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliwapiku mshambuliaji Emmanuel Okwi wa Simba na kiungo Pius Buswita anayecheza nae Yanga kwenye kinyang’anyiro hicho.

Tshishimbi alifunga mabao matatu na kusaidia moja mwezi Fubruari kitu ambacho kilimfanya kuibuka kidedea.

Mkongomani huyo atapewa kitita cha pesa taslimu milioni moja, ngao na kisimbuzi cha Azam TV kama sehemu ya zawadi hiyo.

Tshishimbi anakuwa mchezaji wa pili kutoka Yanga kuchukua tuzo hiyo baada ya Obrey Chirwa msimu huu.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *