Ubungo Wampa Mtaa Victor Wanyama

KIUNGO wa Tottenham Hotspur Mkenya Victor Wanyama amepewa heshima na uongozi wa kata ya Ubungo kwa kushirikiana na chama cha soka wilayani humo (UFA) ya jina la mtaa (Wanyama Street) uliokuwa ukiitwa Viwandani kwenye barabara inayotoka Shekilango kuelekea Uwanja wa Kinesi.

Wanyama ambaye yupo nchini kwa mapumziko baada ya ligi ya Uingireza kumalizika alikuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Ndondo Cup kati ya Kauzu FC dhidi ya Faru Jeuri.

Wakati wa mapumziko wa mchezo huo Wanyama akiambatana na viongozi wa UFA, chama cha soka mkoa (DRFA) na viongozi wa Serikali walitoka nje kwa ajili ya kufanya uzinduzi wa barabara na mtaa huo.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo Wanyama ameishukuru UFA kwa zawadi hiyo huku akisema ni heshima kubwa ambayo hataisahau.

“Nashukuru sana kwa heshima hii mliyonipa ni jambo kubwa la kihistoria katika maisha yangu ambalo nashindwa hata nieleze vipi,” alisema Wanyama.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *