UFARANSA YATANGULIA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA

Timu ya taifa ya Ufaransa imekuwa ya kwanza kuingia nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kuifunga Uruguay mabao 2-0.

Ufaransa ambayo mara ya mwisho kutwaa ubingwa huo ilikuwa mwaka 1998 ilionyesha dhamira ya kuhitaji nafasi hiyo tangu mwanzoni mwa mchezo kutokana na mashambulizi iliyofanya.

Mlinzi Raphael Varane aliifungia Ufaranda bao la kwanza dakika ya 40 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa adhabu wa Antoine Griezmann.

Griezmann alipigilia msumari wa mwisho katika jeneza la Uruguay kwa kufunga bao la pili dakika ya 61 kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Uruguay Fernando Muslera.

Ufaransa itakutana na Brazil au Ubelgiji katika mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *