UINGEREZA YAKIMBIZA MWIZI KIMYA KIMYA, YATINGA NUSU FAINALI

Timu ya taifa ya Uingereza ‘Three Lions’ imetinga nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kuifunga Sweden mabao 2-0.

Uingereza imekuwa timu ya tatu kuingia hatua hiyo baada ya Ufaransa na Ubelgiji kufanya hivyo jana.

Mchezo huo ulianza taratibu huku timu zote zikicheza kwa tahadhari ili kutoruhusu bao la mapema ambalo lingewatoa mchezoni.

Mlinzi Harry Maguire aliifungia Uingereza bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 30 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Ashley Young.

Uingereza iliongeza bao la pili dakika ya 59 kupitia kwa Dele Alli kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Jesse Lingard.

Vijana hao wa kocha Gareth Southgate inasubiri mshindi kati ya Croatia dhidi ya wenyeji Urusi.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *