Ujerumani Mabingwa wa Kombe la Mabara

MOSCOW, Urusi
UJERUMANI imetawazwa mabingwa wapya wa kombe la mabara baada kuifunga Chile bao moja katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye uwanja wa Saint Petersburg nchini Urusi.

Ujerumani walikuwa hawapewi nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo kutokana na kocha Joachim Low kuchagua wachezaji vijana na kuwaacha nyota wake wote waliotwaa kombe la dunia mwaka 2014 hali iliyopelekea kukosolewa vikali kabla michuano hiyo kuanza nchini Urusi mwezi uliopita.

Vijana hao waliokuwa wakiongozwa na nahodha Julian Draxler waliweza kuwadhibiti Chile waliokuwa wakiongozwa na nyota kama Alexis Sanchez, Arturo Vidal na Claudio Bravo.

Lars Stindl aliifungia Ujerumani bao hilo pekee dakika ya 20 baada ya kumalizia kazi safi iliyofanywa na Timo Warner aliyewazidi ujanja mabeki wa Chile na kumpiga chenga mlinda mlango Bravo kabla ya kutoa pasi kwa mfungaji.

Draxler amechaguliwa mchezaji bora wa mashindano wakati Warner akiibuka mfungaji bora kwa kupachika mabao matatu huku Bravo akitwaa tuzo ya kipa bora.

Ujerumani imerudisha taji hilo barani Ulaya kutoka kwa Brazili walilolitwaa mwaka 2014 nchini mwao.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *