UJUMBE WA MO KWA WACHEZAJI WA SIMBA

Baada ya kushinda zabuni katika klabu ya Simba, Mohammed Dewji amewataka wachezaji wa Wekundu hao kutambua thamani ya jezi za Wekundu hao kwa kujituma zaidi uwanjani.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tuhuma za baadhi ya wachezaji kushindwa kujituma hivyo kuikosesha timu ushindi wa makusudi na kuwaumiza mashabiki na wanachama kitu ambacho Mo amewataka nyota hao kukifahamu.

Mo amesema wachezaji wanapaswa kujituma zaidi uwanjani kutafuta matokeo mazuri na kutambua thamani ya jezi wanazo vaa ili kutoa mchango wao kuisaidia Simba kufanya vizuri.

“Wachezaji wanapaswa kutambua ukubwa na thamani ya jezi ya Simba, wakiingia uwanjani wanatakiwa wajitoe mpaka tone la mwisho kuwapa raha mashabiki pamoja na wanachama,” alisema Mo.

Mfanyabiasha huyo ameahidi neema kubwa kwa klabu hiyo huku akitenga kiasi cha sh bilioni moja kwa ajili ya usajili katika mwaka wake wa kwanza na milioni 500 kuboresha benchi la ufundi.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *