UKAME WA MABAO WAMTOA YAHAYA MOHAMED AZAM FC

Uongozi wa klabu ya Azam umethibitisha kuachana na mshambuliaji wake Yahaya Mohammed raia wa Ghana baada ya kushindwa kufunga mabao tangu kuanza kwa msimu huu.

Mshambuliaji huyo amefunga bao moja tu katika michezo tisa ya ligi mpaka sasa hali iliyopelekea uongozi kukaa nae chini kusitisha mkataba wake.

Yahaya amekuwa akiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara kitu ambacho kimepunguza kasi ya mchezaji huyo katika kufumania nyavu.

Msemaji wa klabu hiyo Jaffer Idd amesema kuwa jana uongozi wa Azam ulikutana na mchezaji huyo na kukubaliana kuvunja mkataba ambao ulikuwa wa miaka miwili.

“Kuanzia sasa hatutaendelea na mchezaji wetu Yahaya Mohammed, tumekubaliana kuvunja mkataba na kila kitu kimeenda sawa ataondoka leo kuelekea kwao Ghana,” alisema Jaffer.

Msemaji huyo amesema kuwa uongozi uko mbioni kutafuta mbadala wa mchezaji huyo katika siku chache zijazo.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *