UMTITI AIPELEKA UFARANSA FAINALI KOMBE LA DUNIA

Bao pekee la mlinzi Samwel Umtiti limetosha kuipeleka fainali timu ya Ufaransa baada ya kuifunga Ubelgiji katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa katika uwanja wa St. Petersburg.

Beki huyo wa Barcelona alifunga bao hilo kwa kichwa dakika ya 51 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Antoine Griezmann.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu huku walinda milango Hugo Lloris na Thibaut Cortious wakionyesha umahiri mkubwa.

Vijana hao wa kocha Didier Deschamps wameweka rekodi ya kuwa wakwanza kuingia hatua ya 16 bora, robo fainali, nusu fainali na fainali.

Ufaransa inasubiri mshindi kati ya Uingereza na Croatia ambazo zitakutana kesho katika mchezo wa nusu fainali ya pili.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *