United, Madrid maumivu Marekani

TIMU za Manchester United na Real Madrid zimeambulia vipigo katika mechi zake za International Champions Cup zilizochezwa mapema leo.

United walikuwa wa kwanza kuonja joto ya jiwe baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Barcelona kwenye mchezo ulioanza majira ya saa 8:30 usiku wa kuamkia leo.

Neymar anayehusishwa kutimka klabuni hapo na kwenda zake PSG ya Ufaransa alifunga bao hilo pekee akimalizia pasi ya Lionel Messi.

Neymar akiwatoka walinzi wa United

Majira ya saa 12:30 asubuhi hii pambano lingine lilianza likiwakutanisha matajiri wawili Manchester City ya Pep Guardiola na Real Madrid inayonolewa na Zinedine Zidane.

Katika mechi hiyo City walifanikiwa kuwamiliki Madrid kwa asilimia kubwa na kufanikiwa kuwabugiza jumla ya mabao 4-1

Nicholas Otamendi aliitanguliza City kwa bao la kwanza dakika ya 52 kabla ya winga Raheem Sterling kufunga bao la pili dakika saba baadaye.

Wachezaji wa City wakishangilia moja ya mabao yao dhidi ya Madrid

John Stones aliifungia City bao la tatu dakika ya 67 huku Brahim Diaz akihitimisha karamu hiyo kwa bao la nne dakika ya 82. Bao la kufutia machozi la Madrid liliwekwa nyavuni na Oscar Rodriguez dakika ya 90.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *