United wampa ‘gwala’ Fellain

MANCHESTER, Uingereza
KIUNGO Marouane Fellaini amechaguliwa mchezaji bora wa mechi wa Manchester United baada ya kuonyesha uwezo mkubwa katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya FC Basel kwenye uwanja wa Old Trafford usiku wa jana.

Fellain ambaye anavaa jezi namba 27, aliingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya nahodha wa mchezo huo Paul Pogba aliyepata maumivu kipindi cha kwanza na kushindwa kuendelea na mchezo. Fellain alifunga bao la kwanza kwa kichwa na limekuwa bao la 100 katika michuano ya klabu bingwa Ulaya kufungwa na mchezaji kutoka Ubelgiji.

Fellaini alipata asilimia 80 ya kura zilizopigwa katika mtandao wa Twitter, Ashley Young alipata asilimia 13 huku Nemanja Matic akipata asilimia saba.

Meneja wa United Jose Mourinho amesema kuwa: “Naendelea kusema vile vile kuhusu Fellaini, ni mchezaji maalum ambaye anakupa vitu vingi uwanjani ni mmoja wa wachezaji muhimu kikosini.”

Kiwango cha Fellaini kilivyozungumziwa na baadhi ya mashabiki wa United katika mtandao wa Twitter…

Pat O’Connell (@oconnell2511990): “Amepata kura yangu kwa kweli, amecheza vizuri tena akitokea benchi.”

Paul Irwin (@bluedogspaul): “Alikuwa kila sehemu ambayo alipaswa kuwepo katika uwanja usiku wa jana.”

Carlos Monyi (@CMonyi): “Amewajibu kwa vitendo wanaompinga, amefunga na kusaidia upatikanaji wa bao jingine. Kazi nzuri.”

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *