URA YAENDELEZA UBABE KWA TIMU ZA BARA, YATINGA FAINALI MAPINDUZI

Klabu ya URA kutoka nchini Uganda imetinga fainali ya michuano ya Mapinduzi baada ya kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penati 5-4 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza.

Miamba hiyo ya Uganda tayari imezifunga timu tatu kutoka Tanzania bara kwenye michuano hiyo ambazo ni Azam na Simba katika hatua za makundi kabla ya kuimalizia Yanga hii leo.


Mchezo huo ulilazimika kwenda kwenye hatua za penati baada ya kutoka sare katika dakika 90 za kawaida.

Penati ya mwisho iliyopigwa na mshambuliji Obrey Chirwa ilidakwa na mlinda mlango wa URA na kujikuta wakiondolewa kwenye mashindano hayo.

URA itasubiri mshindi kati ya Azam FC na Singida United ambao watashuka dimbani usiku wa leo katika nusu fainali ya pili kwa ajili ya mechi ya fainali.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *