Urusi Yakubali Kichapo Nyumbani

MOSCOW, Urusi
WENYEJI wa michuano ya kombe la mabara timu ya Urusi imekubali kichapo cha bao moja kutoka kwa Ureno katika mchezo wake wa pili wa kundi A wa mashindano hayo yanayoendela nchini humo.

Urusi walikuwa wanaongoza kundi hilo kufuatia ushindi wa mabao 2-0 walioupata dhidi ya New Zealand katika mchezo wa awali lakini kipigo hicho kimeishusha hadi nafasi ya pili baada ya Ureno kufikisha pointi nne.

Ronaldo akifunga bao pekee katika mchezo huo

Nyota Cristiano Ronaldo alifunga bao hilo pekee kwa kichwa dakika ya nane baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Raphael Guerrero.

Katika mchezo huo wenyeji hawakuwa wazuri kama ilivyokuwa katika mchezo dhidi ya New Zealand hasa kipindi cha kwanza huku Ureno wakiwa bora zaidi kwa kumiliki mpira.

Mexico itacheza na New Zealand katika mchezo wa pili wa kundi hilo majira ya saa 3 usiku huu.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *