Van Dijk aisafishia njia Liverpool

MERSEYSIDE, Uingereza
KLABU ya Liverpool inajiandaa kutoa dau la paundi 60 milioni kwa ajili ya beki wa Southampton Virgil Van Dijk baada ya mlinzi huyo kuomba kuondoka klabuni hapo.

Beki huyo aliandika barua ya kuomba kuondoka akisema:

“Ningependa klabu ya Southampton kufikiria ofa kutoka kwa klabu kubwa kama bado zipo”.

Van Dijk

Liverpool baada ya kuonesha kukata tamaa na usajili wa beki huyo wamepata habari za kuwapa nguvu na kuweza kurejea kuandaa dau hilo ambalo huenda Southampton wakaridhia na kumuachia mlinzi huyo.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *