VERANE: NI NGUMU KUPATA MBADALA WA ZIDANE

Mlinzi wa kati wa timu ya Real Madrid, Raphael Varane amekiri kuwa itakuwa ngumu kupata mbadala wa kocha Zinedine Zidane ambaye ameamua kuachia ngazi.

Varane amesema zinahitaji sifa za ziada kupata mbadala wa Mfaransa huyo aliyedumu na Madrid kwa miaka miwili na nusu akitwaa mataji tisa.

Meneja wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino na Massimiliano Allegri wa Juventus wanapewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya Zidane katika dimba la Santiago Bernabeu.

“Meneja ajae anatakiwa ajue sio kazi rahisi kuifundisha Madrid, ni kazi yenye presha kubwa.

“Zidane amefanya kazi kubwa, ni jambo gumu kurudiwa katika siku za karibuni kitu alichofanya ndani ya miaka miwili na nusu.

“Hatuwezi kumwambia Meneja mpya kuwa tunahitaji kupata mataji mengi kwa muda mfupi ila anapaswa kuendana na mazingira ya Madrid,” alisema Varane.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *