VIBONDE WA EPL WAIPA UBINGWA MAN CITY

West Bromwich Albion walio mkiani mwa msimamo wa ligi kuu Uingereza imeipa ubingwa Manchester City msimu wa 2017/18 baada ya kuifunga Manchester United bao moja katika uwanja wa Old Trafford.

Joe Rodriguez ndiye aliyepeleka kilio kwa vijana hao wa kocha Jose Mourinho baada ya kufunga bao hilo dakika ya 73.

Licha ya ushindi huo West Brom imefikisha pointi 24 huku wakionekana itakuwa ngumu kunusurika na janga la kushuka daraja.

Kipigo hicho kinaifanya United kubaki na pointi 71 ikizidiwa alama 16 na City yenye pointi 87 ambapo katika michezo mitano iliyobaki haiwezi kufikisha alama hizo.

Manchester City mabingwa wapya wa msimu wa 2017-2018
Hii ina maana Man City inayonolewa na kocha Pep Guardiola imepata taji la pili msimu huu baada ya lile la Carabao iliyopata kwa kuifunga Arsenal mabao 3-0 katika mchezo wa fainali.

United sasa inaizidi Liverpool alama moja iliyo nafasi ya tatu lakini ikiwa na faida ya mechi moja mkononi.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *