Viingilio Stars dhidi ya Malawi “bwerere” kabisa.

Timu ya taifa ya Tanzania maarufu kama Taifa stars leo hii inajitupa kiwanjani kupambana na timu ya taifa la Malawi, mchezo utakaopigwa majira ya jioni.

Viingilio kutazama mchezo huo ni shilingi elfu tano ( 5,000) kiwango cha juu na shilingi elfu tatu ( 3,000) kiwango cha chini kabisa.

Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, limewaomba wapenda soka na wananchi wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kiwanjani kuipa nguvu stars ili iweze kuibuka na ushindi na kupanda ngazi katika viwango vya FIFA.

Kwa upande wake mwalimu wa stars, Salum Mayanga amesema atautumia mchezo huo kama jaribio na kupata picha kamili kuelekea kwenye mechi za kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Africa (AFCON).

Katika kuhakikisha watanzania wanapata taarifa kamili juu ya mchezo huo, matangazo kadhaa yamefanyika kwa wiki nzima ikiwemo burudani za miziki katika maeneo tofauti tofauti jijini Dar es salaam.

kikundi cha burudani kikitangaza mchezo wa Stars dhidi ya Malawi
It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *