WANAHABARI WA BARA WAWASHIKISHA ADABU WENZAO WA ZENJI

Timu ya Waandishi wa habari za michezo kutoka Tanzania bara wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenzao kutoka Zanzibar katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Amani.

Waandishi hao wapo visiwani humo kuripoti michuano ya kombe la Mapinduzi ambayo leo imesimama kupisha sherehe za Mapinduzi zilizofanyika kwenye uwanja huo.


Katika mchezo huo mabao ya bara yalifungwa na Anuari Binde aliyefunga mawili na Abducardo Emmanuel.

Waandishi wa bara walitawala sehemu kubwa ya mchezo huo wakitengeneza nafasi kadhaa za kufunga zaidi ya wapinzani wao.

Mchezo wa fainali wa michuano ya Mapinduzi utafanyika kesho saa 2 usiku kati ya Azam FC dhidi ya URA.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *