Wapya wafanya vitu vya hatari kuinogesha Simba Day

NYOTA wapya wa timu ya Simba Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima na Nicholas Gyan wamekonga nyonyo za mashabiki wa Wekundu hao baada ya kuonyesha soka safi wakiibuka na ushindi wa bao katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda kwenye uwanja wa Taifa.

Mchezo huo maalum wa tamasha la Simba Day hutumiwa na klabu ya Simba kutambulisha jezi mpya za msimu pamoja na wachezaji huku nyota hao watatu wakishangaliwa kila wagusapo mpira.

Haruna Niyonzima akimtambuka mlinzi wa Rayon

Mohammed Ibrahim aliipatia Simba bao la kwanza dakika ya 15 baada ya kupokea pasi ya Okwi ndani ya eneo la 18 kufuatia kuwazidi ujanja mabeki wa Rayon.

Simba ilitawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza kwa kufanya mashambulizi mengi lakini Rayon walizinduka dakika ya 31 kwa kuliandama lango la Wekundu hao baada ya kutokea piga nikupige lakini vijana wa kocha Joseph Omog walizima jaribio hilo.

Emmanuel Okwi alicheza kwa dakika 45 tu lakini mashabiki walifurahia ‘show’

Kipindi cha pili kocha Omog aliiwaingiza Jonas Mkude, Nicholas Gyan, Haruna Niyonzima, Ally Shomari, Mwinyi Kazimoto na Said Ndemla ambao waliongeza kasi na kulifanya lango la Rayon kuwa shakani muda wote.

Pamoja na mshambulizi mengi yaliyofanywa na wachezaji hao, Simba ilishindwa kuongeza mabao mengine kutokana washambuliaji kushindwa kutumia nafasi nyingi walizopata.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *