Wasauzi washindwa dau la Juuko, kutua nchini wiki ijayo

BEKI wa kati wa timu ya Simba, Juuko Murshid atawasili nchini wiki ijayo kujiunga na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu baada ya timu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini kushindwa kufikia makubaliano na Wekundu hao.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na taarifa za beki huyo raia wa Uganda kutaka kutimkia Afrika Kusini kujiunga na miamba hiyo lakini wameshindwa kufikia dau linalotakiwa na mabingwa hao wa kombe la FA.

Juuko Murshid

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa beki huyo atawasili nchini wiki ijayo na kujiunga na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya ligi kwakua bado wana mkataba nae.

“Juuko ni mchezaji wa Simba bado ana mkataba, atawasili nchini wiki ijayo na atajiunga moja kwa moja na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya ligi,” alisema Manara.

Haji Manara, msemaji Simba SC

Wakati huo huo Manara amesema kuwa mkutano mkuu wa klabu hiyo utafanyika kesho saa 4 asubuhi katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere International Conference Center uliopo Posta, Dar es Salaam baada ya Mahakama kutupilia mbali ombi la zuio lililopelekwa na baraza la wadhamini wa Wekundu hao.

Juzi Alhamisi baraza la wadhamini wakiongozwa na Mzee Hamis Kilomoni walienda hahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuzuia mkutano huo kutokana na viongozi wakuu wa klabu hiyo Rais Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange kushikiliwa na vyombo vya dola kwa tuhuma za utakatishaji fedha.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *