Washambuliaji Simba ‘waanza’ na Gulioni

SAFU ya ushambuliaji ya Simba imeanza kujibu mapigo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya timu ya Gulioni FC katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Amani, visiwani Zanzibar.

Katika mechi za kujipima nguvu za kujiandaa na msimu mpya wa ligi pamoja na mchezo wa ngao ya jamii Simba imekuwa na tatizo katika umaliziaji licha ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga na kucheza soka safi.

Simba imefanya usajili wa nyota wenye majina makubwa kama Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima, John Bocco, Nicholas Gyan lakini changamoto imekuwa katika ufungaji.

Katika michezo mitano ya kirafiki dhidi ya timu za Orlando Pirates, Bidvest (zote za Afrika Kusini), Rayon Sports ya Rwanda, Mtibwa Sugar na Mlandege ya Zanzibar Simba ilifunga mabao matatu pekee.

Katika mchezo huo uliomalizika muda mfupi uliopita mabao ya Simba yalifungwa na Laudit Mavugo aliyefunga mawili, Juma Liuzio, Mohammed Ibrahim na Shiza Kichuya.

Simba itakutana na watani wake wa jadi Yanga Jumatano ya Agosti 23 katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa ngao ya hisani kuashiria kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu ya Vodacom.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *