Wazee Simba Watia Timu kwa Magufuli

WAZEE wa klabu ya Simba wameazimia kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli ili kumweleza kuhusu taarifa za baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali kushinikiza klabu hiyo kuuzwa kwa mfanyabiasha Mohammed Dewji ‘Mo’.

Kauli hiyo inakuja siku chache baada ya klabu hiyo kusaini mkataba wa udhamini na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa ambapo baadhi ya viongozi na wadau wa klabu hiyo hawakukubaliana na suala hilo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mratibu wa wazee wa wanachama wa Simba Felix Makuwa alisema wameamua kwenda kwa Rais Magufuli ili awasaidie kwa kuzuia mchakato huo usiendelee kwa manufaa ya klabu yao.

PicsArt_05-17-11.33.19

“Tumeshaandika barua ya kutaka kuonana na Rais Magufuli kupitia Waziri mwenye dhamana ya michezo Harrison Mwakyembe kwavile hatuko tayari kuona klabu yetu iliyotulea furaha inauzwa,” alisema Makuwa.

Kwa upande wake Chuma Suleiman ‘Bi Hindu’ alisema suala la hisa halikubaliki ndani ya klabu hiyo na wanampongeza Rais wa Simba Evans Aveva kwa kuingia mkataba mnono na SportPesa ambao ni msaada mkubwa kwa klabu hiyo.

“Sisi ndiyo wenye Simba yetu hao wote watoto wamekuja juzi kwahiyo hawawezi kutupokonya klabu yetu,” alisema Bi Hindu

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *