Wenger aanza na taji Uingereza

LONDON, Uingereza
KOCHA Arsenal, Mfaransa Arsene Wenger ameanza vema msimu huu baada ya kushinda ngao ya hisani kwa kuifunga Chelsea kwa mikwaju ya penati 4-1 katika uwanja wa Wembley kufuatia sare ya bao moja kwenye muda wa kawaida.

Mchezo huo unaashiria kungufuliwa kwa pazia la ligi kuu nchini Uingereza ambapo wikiendi ijayo kampeni za kumsaka bingwa mpya kwa msimu wa 2017/18.

Chelsea walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na kiungo Victor Moses dakika ya 46 baada ya kupokea pasi kutoka kwa beki Garry Cahill.

Mwamuzi alimtoa Pedro kwa kadi nyekundu dakika ya 80 baada ya kumchezea rafu kiungo Mohammed Elneny.

Beki mpya Saed Kolasinac aliisawazishia Arsenal kwa kichwa dakika ya 82 baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Granit Xhaka.

Penati za Arsenal zilifungwa na Theo Walcott, Nacho Monreal, Alex Chamberlain na Oliver Giroud wakati Cahill alifunga penati ya Chelsea huku Thibaut Courtious na Alvaro Morata wakikosa mikwaju yao.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *