WENGER AITOLEA ‘POVU’ MAN CITY, ASEMA INAFUNGIKA

Meneja Arsene Wenger ameitolea povu Manchester City akisema timu hiyo inafungika huku akimlaumu mwamuzi kuwa alikuwa sehemu ya kipigo cha mabao 3-1 walichokipata Arsenal mwezi uliopita kutoka kwa wababe hao.

City ipo kwenye kiwango bora kwa sasa kulinganisha na ‘Washika bunduki’ hao ambao Jumamosi ijayo watacheza na Tottenham Hotspur, baada ya kushinda mechi 10 katika michezo 11 ya ligi mpaka sasa.

Asernal wapo nafasi ya sita wakiwa nyuma kwa pointi 12 dhidi ya vijana hao wa Pep Guardiola lakini Wenger amesisitiza City wanaweza kufungwa.

“City wako vizuri lakini wanafungika. Katika mchezo dhidi yetu hawakuwa wametuzidi sana, mchezo ulikuwa mgumu pande zote
“Walitengeneza nafasi chache, walituzidi shuti moja tu lililolenga goli,” alisema Wenger.

Wenger alimlaumu mwamuzi Michael Oliver kukubali bao la tatu la City lililofungwa na Gabriel Jesus ambaye alikuwa ameotea.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *