Wenger akubali Arsenal ilikuwa kimeo jana

MERSEYSIDE, Uingereza
KOCHA wa Arsenal mfaransa, Arsene Wenger amebainisha kuwa kiwango cha wachezaji wake kilikuwa chini na kufanya makosa mengi hali iliyopelekea kupokea kipigo kikubwa katika uwanja wa Anfield jana.

Wenger amesema kipigo cha mabao 4-0 walichokipata toka kwa Liverpool kilisababishwa na kiwango kibovu cha wachezaji wake ambao walishindwa kujituma.

Mabao ya Liverpool yalifungwa na Roberto Firmino (17) na Sadio Mane (40) huku Mohamed Salah akiongeza la tatu dakika ya 57 na Daniel Sturridge akimalizia la mwisho dakika ya 77.

“Matokeo yametokana na kiwango chetu duni, hatukuwa bora kabisa. Tulizidiwa kila mahali wenzetu pia walitumia nguvu, tulifanya mchezo kuwa rahisi kwa Liverpool tukafanya makosa mengi,” Wenger aliiambia Sky Sports.

“Tulianza kwa kumiliki mpira kipindi cha pili lakini goli la tatu lilimaliza mchezo, ilikuwa ngumu kwetu lakini tulikuwa katika kiwango kibovu mno.

“Ilitushtua kwa goli la Mane kabla ya kwenda mapumziko ila hatupaswi kulalamika sana tunahitaji muda kukaa sawa na kipindi hiki wachezaji wanakwenda katika mapumziko ya mechi za kimataifa lakini nikiri kuwa tulikuwa katika kiwango kibovu mno,” alimaliza Wenger.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *