WENGER AMPONZA WILSHERE TIMU YA TAIFA

Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza,Gareth Southgate ametangaza kumuacha kiungo Jack Wilshere kwenye kikosi chake kutokana na kuchezeshwa nafasi tofauti katika timu yake ya Arsenal ukilinganisha na majukumu anayotaka kumpa kwenye timu ya taifa.

Ruben Loftus-Cheek, kinda wa Chelsea anaechezea Crystal Palace kwa mkopo atacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Ujerumani usiku wa leo huku viungo Jack Cork wa Burnley na Jake Livermore wa West Bromwich Albion wakiitwa badala ya Wilshere.

Southgate amefafanua sababu ya kumuacha Wilshere kwenye kikosi chake ni kutokubali jinsi ambavyo kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anavyomtumia.

Jack anacheza namba 10 kwa muda wote alipokuwa kwa mkopo Bournemouth msimu uliopita, lakini sisi hatuchezi aina hiyo. Tukicheza na mchezaji namba 10 basi tunae Dele Alli na Adam Lallana.

Sidhani kama Jack ni namba 10, yeye ni kiungo wa chini na anafanya vizuri zaidi katika nafasi hiyo lakini hachezeshwi chini nafikiri mkimuuliza Wenger atakuwa na majibu.

Niweke wazi kuwa namkubali sana Jack, ana kipaji cha hali ya juu na nina muheshimu pia nina matumaini mwezi Machi naweza kumjumuisha kikosini.” alisema Southgate.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *