WENGER ANA MATUMAINI YA OZIL KUIVAA CITY JUMAPILI

Meneja Arsene Wenger ana matumaini kibao juu ya kiungo wake Mesut Ozil atakuwa fiti na anatarajia kuwepo kwenye mchezo wa fainali wa Carabao dhidi ya Manchester City siku ya Jumapili.

Mjerumani huyo aliugua homa na alikosa mchezo wa Europa Alhamisi iliyopita dhidi ya Ostersund nchini Sweden na leo usiku watarudiana kwenye uwanja wa Emirates.

Vijana wa Wenger wana mtaji wa mabao matatu waliopata kwenye mchezo wa awali, ingawa Ozil atakosa pia mchezo wa leo lakini kuna uwezekano mkubwa wa kushuka dimbani siku ya Jumapili.

“Mfumo wake wa kinga ya mwili unamsumbua sijui inasababishwa na nini, matumaini yetu atakuwa fiti kabla ya kukutana na Man City Jumapili.

“Leo amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza, ningeweza kumtumia leo lakini kwakua anaumwa Jumapili anaweza kujumuishwa kikosini,” alisema Wenger.

Wenger amethibitisha kuwa mlinda mlango David Ospina atakuwa golini kwenye uwanja wa Wembley kufuatia Petr Cech kuendelea kuwa majeruhi.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *