WENGER ATAJA SABABU ZA UBUTU WA LACAZETTE

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwasili kwa mshambuliji Pierre-Emerick Aubameyang ni moja ya sababu ya Alexandre Lacazette kuwa butu.

“Lacazette anapitia kipindi kigumu sasa kuliko ilivyokuwa awali, anajituma sana mazoezini na anafunga vizuri lakini sijui kitu gani kinamtokea uwanjani.

“Huwa inatokea lakini nadhani hali ya kujiamini ni tatizo kwake ikichangiwa na ujio wa Aubameyang kwakua kumeongezeka ushindani.

Gwiji wa zamani wa Washika bunduki hao, Emmanuel Petit amesema usajili wa Auba unamaanisha maisha ya Lacazette ndani ya Arsenal yapo shakani.

Muda utazungumza kama mshambuliji huyo wa zamani wa Olympique Lyon ataweza kuhimili mikikimikiki ya ligi kuu nchini Uingereza.

Raia huyo wa Ufaransa tayari amefunga mabao tisa kwenye ligi kuu nchini humo.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *