Ya Brazil yawageukia Argentina Ecuador.

TIMU ya taifa la Argentina leo hii imetua katika ardhi ya Ecuador chini ya usimamizi wa kijeshi, wakiwa katika hatari kubwa ya kukosa kushiriki michuano ya kombe la dunia nchini Urusi.

Argentina itaceheza na Ecuador katika dimba la Olimpico Atahualpajijini Quito, ulioko umbali wa mita 2,782 kutoka usawa wa bahari.Argentina haijawahi kupata ushindi katika uwanja huo katika kipindi cha takribani miaka 16.

Uwanja wa Olimpico Atahualpa ulioko umbali wa mita 2,782 kutoka usawa wa bahari.

Tatizo la kucheza kwenye viwanja vilivyopo juu kutoka usawa wa bahari liliikumba Brazil juma lililopita na kuisababisha kupatiwa msaada wa gesi kwa ajili ya kurahisisha upumuaji katika mchezo wao dhidi ya Bolivia.

Ushindi dhidi ya Ecuador ni muhimu kwa Argentina kama wanataka kupata nafasi ya kushiriki kombe la dunia mwakani huku ikiiombea Peru kupoteza mchezo wao dhidi ya Colombia.Argentina inashika nafasi ya 6 ikiwa na alama 25 nyuma ya Peru yeneye alama 25,lakini ikiwa juu kwa idadi kubwa ya magoli ya kufunga.

Msimamo wa kundi la Amerika ya kusini.

kukosa ushindi katika mchezo huo utamaanisha Urusi na dunia itakosa burudani ya wachezji bora duniani kama vile Dyabala, Higuain,Aguero, Di maria lakini pia unaweza kua ndio mwisho wa kumuona Lionel Messi katika michuano ya kombe la dunia.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *