YANGA KAMILI KUWAFUATA ST LOUIS KESHO

Msafara wa watu 30 wa mabingwa watetezi wa ligi kuu timu ya Yanga utaondoka kesho asubuhi kuelekea visiwa vya Shelisheli kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi St Louis utakaofanyika Jumanne ya Februari 20.

Katika msafara huo wachezaji ni 20 wakati benchi la ufundi likiwa na watu nane na viongozi wawili wa Kamati ya Utendaji.

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Dismas Ten amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kinacho subiriwa ni muda tu ufike kwa ajili ya safari.

“Kikosi kitaondoka kesho na wachezaji 20 benchi la ufundi watu nane na viongozi wawili wa Kamati ya Utendaji,” alisema Ten.

Ten amewataja nyota Donald Ngoma, Amiss Tambwe, Yohana Nkomola na Abdallah Shaibu kuwa hawatasafiri na timu kutokana na kuwa majeruhi.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *