YANGA KUREJEA USIKU WA LEO

Mabingwa wa Tanzania timu ya Yanga itarejea saa tatu usiku wa leo ikitokea visiwani Shelisheli ilipokuwa na mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika dhidi ya St Louis.

Yanga ililazimishwa sare ya bao moja jana na wenyeji St Louis lakini wakifanikiwa kutinga hatua ya kwanza ya michuano hiyo kwa jumla ya mabao 2-1 kufuatia ushindi wa bao mojakwa bila katika mechi ya kwanza.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa mabingwa hao Hussein Nyika ambaye ameambatana na timu hiyo amesema watarejea saa tatu usiku na kesho watasafiri kuelekea Songea kwa ajili ya mchezo wa FA dhidi ya Majimaji siku ya Jumapili.

“Kikosi kinarejea leo usiku na kinatarajia kusafiri kwenda Songea kesho asubuhi kwa ajili ya mchezo wa FA na baadae tutaenda Mtwara kukutana na Ndanda FC,” alisema Nyika.

Katika mchezo wa hatua ya kwanza Yanga itakutana na Township Rollers ya Botswana ambapo wataanzia jijini Dar es Salaam Machi 6.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *