YANGA KUWAFUATA ROLLERS USIKU HUU

Kikosi cha timu ya Yanga kitaondoka usiku wa leo kuelekea nchini Botswana kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers wikiendi ijayo.

Yanga itasafiri ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kupata ushindi mara mbili mfululizo kwenye ligi wakifunga mabao sita na kuruhusu bao moja pekee dhidi ya Kagera Sugar (3-0) na Stand United (3-1).

Katibu mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa amesema kuwa timu itaondoka usiku wa leo kuelekea Botswana kwa ajili mchezo huo ambao amekiri utakuwa mkali.

“Kikosi kitaondoka usiku wa leo na wachezaji wote ambao tumekuwa tukiwatumia kwenye michezo yetu ya karibuni na wale majeruhi wataendelea kubaki kwa ajili ya kupata matibabu,” alisema Mkwasa.

Yanga itaingia kwenye mchezo huo utakaofanyika Machi 17 ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 2-1 walichopata kwenye uwanja wa Taifa wiki iliyopita.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *