YANGA ‘NUSU’ YAANZA MITIZI KAUNDA

NA MWANDISHI WETU,

kaundai-stadium-jan21-2013

KIKOSI cha mabingwa wa Ngao ya Hisani, timu ya soka Yanga leo jioni kinatarajiwa kurudi mazoezini kwenye uwanja wao wa Kaunda jijini Dar es Salaam, tayari kabisa kwa maandalizi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Septemba 12.

Yanga itafanya mazoezi hayo ikiwa na nyota wake kadhaa, huku baada ya nyota wengine wakiwa na kikosi cha timu ya taifa nchini Uturuki.

Akizungumza na Simba Makini, asubuhi hii, Meneja mkuu wa kikosi hicho Hafidh Saleh alisema, kikosi chao kitaanza mazoezi hapo kabla ya kesho kuhamia kwenye uwanja wa Polisi Kurasini.

Saleh alisema, wanafahamu watakuwa na idadi ndogo ya wachezaji watakaojitokeza kwenye mazoezi hayo kutokana na wachezaji wengine kuwa na majukumu hayo ya timu ya taifa.

“Leo jioni tutaanza mazoezi yetu kwenye Uwanja wa Kaunda. Tunafahamu tutakuwa na idadi ndogo ya wachezaji ambao watahudhulia, lakini hakuna jinsi zaidi ya kufanya hivi ili tuendelee na program ya kocha Hans Van Pluijm, ambaye ametaka tuanze mazoezi.

“Leo tutakuwa hapa Kaunda, lakini kesho mazoezi yatahamia Uwanja wa Polisi Kurasini ambako tumekuwa tukifanya mazoezi yetu huko mara kwa mara” alisema Saleh.

Katika hatua nyingine Saleh amesema, wachezaji waliopo timu ya taifa wakimaliza mchezo wao na Nigeria Septemba 5, ndio watakusanyika pamoja na kuanza masuala ya kambi ya muda mrefu kuelekea ligi kuu.

 

“Hatuwezi kuingia kambini hivi sasa kutokana na kikosi kutokukamilika, kikosi kitangia kambini rasmi baada ya nyota wetu waliokuwa timu ya taifa kurejea kikosini” alisema.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *