Yanga Waliamsha ‘Dude’ la Usajili

BAADA ya kimya kirefu, mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Yanga wameanza mawindo ya kuandaa kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao baada ya kufanikiwa kupata saini ya beki wa kati Abdallah Hajji kutoka Taifa Jang’ombe ya visiwani Zanzibar.

Beki huyo anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Yanga tangu harakati za usajili zilipoanza ambapo watani wao Simba pamoja na Azam wamekuwa wakifanya usajili kwa wachezaji wengi wenye majina.

Meneja wa klabu Hafidh Salehe ameithibitishia mtandao huu juu ya usajili huo ambapo beki huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuwatumikia mabingwa hao mara tatu mfulululizo.

“Ni kweli tumemsajili beki Abdallah Hajji kutoka Jang’ombe kwa mkataba wa miaka miwili tunaamini atatusaidia,” alisema Hafidh.

Mabingwa hao wamepanga kufanya usajili wa kimya kimya ambapo watakuwa wakitangaza mchezaji baada ya kukamilisha usajili.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *